Unatakiwa utimize vigezo vifuatavyo
• Je kampuni yako imesajiliwa Tanzania?
• Je kampuni yako ni wasindikaji wa mazao ya bidhaa za kilimo?
• Je mauzo yako ni zaidi ya shilingi milioni 200 kwa mwaka?
• Je unafanya kazi kwa karibu na wanaowapatia malighafi?
• Je unaaminika na uko tayari kushiriki taarifa zako za kifedha?
• Je unao uwezo wa kutoa dhamana stahiki kwa ajili ya mkopo?
Kama unakidhi vigezo hivyo hapo juu, Kampuni za kundi la Match Maker wanatazamia kukusaidia kuiimarisha biashara yako. Tafadhali jaza fomu hiyo hapo chini na uitume kwetu. Unaweza pia kuinakili (download) fomu hiyo (ya Kiswahili au kiingereza). Tafadhali jaza fomu hii kwa makini kuhusu taarifa za biashara yako na mkopo unaotarajia na uitume kwa jovitus@mmfm-ltd.com. Utapata majibu yetu katika muda wa wiki mbili.