You are here:
Huduma zetu kwa Biashara za Kati
Mfuko wa SME Impact Fund, unaosimamiwa na MMFM umejiimarisha kutoa mikopo kwa wajasiriamali wa kati kwenye minyororo ya thamani ya sekta ya kilimo. Mfuko unalenga zaidi wale wajasiriamali wa kati ambao huongeza thamani kwenye bidhaa za kilimo na wenye mahitaji ya kifedha kati ya shilingi milioni 100 na shilingi bilioni 1.
Pamoja na kutoa mikopo ili kukuza biashara yako, sisi pia tunakusaidia kuongeza ufahamu wa kina katika biashara yako. Kukuwezesha kifedha pamoja na utambuzi wa kina kuhusu jinsi ya kukuza biashara yako, kutapelekea biashara yako kuwa mahiri na hatimaye kuongeza kipato zaidi mfukoni mwako.